Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 17:51

Hamas yawaambia wapatanishi msimamo wake kuhusu sitisho la mapigano haujabadilika


Balozi wa Israel kwenye Umoja wa mataifa Gilad Erdan akilihutubia Baraza la Usalama la UN baada ya azimio linaloomba sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas kukwama, Machi 22, 2024. Picha ya Reuters
Balozi wa Israel kwenye Umoja wa mataifa Gilad Erdan akilihutubia Baraza la Usalama la UN baada ya azimio linaloomba sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas kukwama, Machi 22, 2024. Picha ya Reuters

Kundi la Hamas Jumatatu liliwambia wapatanishi kwamba litaendelea kushikilia msimamo wake wa awali kuhusu kufikia makubaliano ya sitisho la mapigano la kudumu, ikiwemo kuwaondoa wanajeshi wa Israel ndani ya Gaza na kurejea nyumbani kwa Wapalestina waliyolazimishwa kuhama makazi yao.

Limeomba pia kile linachoita “ubadilishaji wa ukweli wa wafungwa”, likimaanisha wafungwa wa Kipalestina kutoka magereza ya Israel kwa kubadilishana mateka wa Israel wanaoshikiliwa Gaza.

Hapakuwa maelezo ya mara moja kutoka kwa ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Hamas iliwasilisha pendekezo lake kuhusu sitisho la mapigano kwa wapatanishi na Marekani katikati mwa mwezi Machi ambalo lilijumuisha kuachiliwa kwa mateka wa Israel kwa kubadilishana na kuachiwa huru kwa wafungwa wa Palestina, 100 kati yao ambao wanatumikia vifungo vya maisha gerezani, kulingana na pendekezo hilo ambalo Reuters ilifaulu kuliona.

Baraza la Usalama la Umoja mataifa Jumatatu lilipitisha azimio linaloomba sitisho la mapigano la mara moja kati ya Israel na Hamas baada Marekani kujizuia kupiga kura, hali ambayo imeleta mtafaruku na mshirika wake Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG