Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 15, 2025 Local time: 13:49

Hamas yakabidhi mateka 3 kwa Israel


Hamas iliwakabidhi mateka watatu wa Israel, Jumamosi, ikiwa ni mfululizo wa mabadilishano  ya karibuni katika makubaliano yenye lengo la kumaliza mzozo kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Palestina.

Mfaransa mwenye asili ya Israel, Ofer Kalderon, 54, na Yarden Bibas, 35, walikabidhiwa kwa chama cha Msalaba Mwekundu katika mji wa kusini mwa Gaza wa Khan Younis, kabla ya kurejeshwa Israeli.

Muisraeli mwenye asili ya Mmarekani, Keith Siegel, 65, aliachiliwa saa chache baadaye katika bandari ya Gaza City.

Bibas alichukuliwa kutoka Kibbutz Nir Oz wakati wa shambulizi la kigaidi la Hamas la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israeli pamoja na mkewe, Shiri, na wavulana wao wawili, Ariel, 5, na Kfir, 2.

Hatima ya familia yake haijulikani mpaka sasa.

Siegel, anayetokea Chapel Hill, North Carolina, alichukuliwa mateka Kibbutz Kfar Aza pamoja na mkewe, Aviva Siegel.

Aviva Siegel aliachiliwa wakati wa sitisho la muda mfupi la mapigano mnamo Novemba 2023.

Forum

XS
SM
MD
LG