Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 19:39

Hali yazidi kuwa tete Misri


wananchi wa Misri wakiandamana karibu na majengo ya bunge mjini Cairo.

Wananchi wanaokiunga chama cha Muslim Brotherhood wakusanyika Tahrir Square kuitaka tume ya uchaguzi kutangaza matokeo ya urais.

Huko Misri, maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono chama cha kiislam cha Muslim Brotherhood Ijumaa walikusanyika katika uwanja wa Tahrir Square mjini Cairo, kupinga kile wanachosema ni unyakuzi wa madaraka uliofanywa na watawala wa kijeshi nchini humo na kutoa mwito wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa marudio yaliyocheleweshwa mno baada ya kura hiyo wiki jana.

Tume ya uchaguzi ya Misri imeahirisha matokeo ya uchaguzi huo yaliyotazamiwa kutangazwa Alhamis ikisema inahitaji muda wa kupeleleza malalamiko ya wizi wa kura yaliyowasilishwa na pande zote mbili. Chama cha Muslim Brotherhood kimeonya juu ya mzozano kati ya raia na watawala wa kijeshi endapo mgombea wao Mohammed Morsi hatatangazwa kuwa mshindi.

Wote Morsi na waziri mkuu wa zamani Ahmed Shafiq wanadai ushindi katika uchaguzi huo wa marudio na wafuasi wao wametishia kutakuwa na vurugu endapo wagombea wao watashindwa katika kinyang’anyiro hicho. Chombo rasmi cha habari huko Misri MENA kinaripoti kuwa tume ya uchaguzi itatangaza matokeo hayo ama Jumamosi au Jumapili.

XS
SM
MD
LG