Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 13:46

Hali ya vita yaathiri Sudan


Jeshi la Sudan likifanya doria hulo Gedaref Mashariki mwa Sudan, December 18, 2023. Picha na AFP
Jeshi la Sudan likifanya doria hulo Gedaref Mashariki mwa Sudan, December 18, 2023. Picha na AFP

Vita vya Karibu miezi 20  nchini Sudan vimeiweka nchi hiyo katika hali ngumu sana, wakati baadhi ya maeneo yenye mahitaji mkubwa hayafikiwi kabisa ili kuweza kupata mahitaji ya kibinadamu

Vita vya Karibu miezi 20 nchini Sudan vimeiweka nchi hiyo katika hali ngumu sana, wakati baadhi ya maeneo yenye mahitaji mkubwa hayafikiwi kabisa ili kuweza kupata mahitaji ya kibinadamu. Zaidi ya watu milioni 12 wamekoseshwa makazi, zaidi ya milioni nane kati yao wamebaki ndani ya Sudan na zaidi ya milioni tatu wamekimbia katika nchi Jirani.

Tayari Sudan ilikuwa inakabiliwa kwa miaka kadhaa na mzozo mkubwa wa kibinadamu lakini vita hivyo vimesababisha janga kubwa zaidi la kibinadamu haswa kwa wanawake na Watoto. Mamilioni ya watu wameyahama makazi yao , wakikabiliwa na njaa , magonjwa na ghasia.

Hali ni mbaya sana na kuna ripoti za kuenea kwa unyanyasaji wa kijinsia , mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, na njaa kali ikiripotiwa katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam Darfur kaskazini.

Takriban wanawake milioni 2.7 walio katika umri wa kujifungua wamekimbia makazi yao , ikiwa ni Pamoja na zaidi ya wanawake wajawazito 272,000 ambapo karibu wanawake 91,000 watajifungua mwezi ujao.

Inakadiriwa kila siku watu elfu 20 wanakoseshwa makazi miongoni mwao ni wanawake wajawazito wanaokimbia kuokoa Maisha yao na hawawezi kupata huduma za ujauzito , kujifungua salama au huduma za baada ya kujifungua kwa sababu hadi asilimia 80 ya vituo vya afya vimefungwa au havifanyi kazi vizuri katikia maeneo yaliyoathiriwa na mzozo. Kwa matokeo yake wanawake wanakufa kutokana na ujauzito na matatizo yanayohusiana na uzazi.

Kubakwa na kutekwa ni mambo makuu yanayojitokeza katika mzozo huu na wanawake na wasichana bado wanafanyiwa vitendo vya ubakaji , utekaji na kulazimishwa ndoa . idadi ya watu walio katika ukatili wa kijinsia imeongezeka mara dufu tangu kuanza mzozo huu kutoka milioni 6.9 hadi milioni 12.2 . kukiwa na asilimia 400 iliyoongezeka kwa watu wanaotafuta huduma za GBV katika miezi sita iliyopita.

Licha ya hali hiyo ngumu UNFPA inafanya kazi kwa bidi kutoa msaada wa kuokoa Maisha , ikiwemo huduma za uzazi kwa wanawake na wasichana wa Sudan lakini inahitaji msaada wa haraka kufanya hivyo. Mwaka 2025 UNFPA inahitaji kwa dharura dola milioni 119.6 kushughulikia mahitaji muhimu ya wanawake na wasichana . Mwaka jana ombi la UNFPA la dola milioni 82 lilijibiwa kwa asilimia 20 tu.

Forum

XS
SM
MD
LG