Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 02:07

Hali ya usalama yaharibika zaidi Afrika ya kati kuelekea uchaguzi mkuu


Vikosi vya kulinda amani katika Jamhuri ya Afrika ya kati

Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu katika jamhuri ya Afrika ya kati, Umoja wa mataifa umesema kwamba kuna ripoti za kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya maafisa wa usalama, wagombea wa viti mbalimbali katika uchaguzi huo na dhidi ya maafisa wanaosimamia uchaguzi.

Makundi yenye silaha yamekabiliana na maafisa wa usalama katika sehemu mbalimbali za nchi hiyo, ikiwemo katika sehemu zilizo karribu na mji mkuu wa Bangii.

Msemaji katika ofisi ya haki za kibinadamu ya umoja wa mataifa Liz Throssell, amesema kwamba wana wasiwasi mkubwa kutokana na ripoti za kuongezeka machafuko kutokana na hasira za kisiasa na uenezaji wa habari za chuki nchini humo.

Amesema kwamba maafisa wa usalama na makundi yenye silaha, Pamoja na maafisa wa kulinda usalama kutoka nje ya nchi hiyo wanatakiwa kuheshimu sheria ya kimataifa na haki za kibinadamu.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, ametoa wito kwa pande zote husika katika mzozo huo Jamhuri ya Afrika ya kati kumaliza ghasia.

Uchaguzi wa urais umevutia wagombea 17 katika uchaguzi huo wa Jumapili Desemba 27.

Rais wa sasa Faustin-Archange Touadera anagombea mhula wa pili madarakani na anatarajiwa kushinda uchaguzi huo.

Aliyekuwa rais Francois Bozize ambaye alionekana kuwa mpinzani mkuu wa Bozize, alizuiliwa na mahakama ya katiba kugombea nafasi hiyo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG