Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 15:10

Mamilioni ya raia wa Ethiopia wahitaji msaada wa chakula


Wanawake wa Ethiopia wakipokea msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya katika eneo la Shinile nchini Ethiopia.
Wanawake wa Ethiopia wakipokea msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya katika eneo la Shinile nchini Ethiopia.

Zaidi wa Ethiopia milioni 10 wanahitaji msaada wa haraka wa chakula kutokana na kuendelea kwa hali ya ukame. Watoto ndio walio katika mazingira hatari zaidi.

Mama mmoja aliyelazwa hospitalini akiwa na mtoto wake wa umri wa miaka 3 mwenye utapia mlo anasema maradhi yaliyompata mwanawe ni sababu ya ukosefu wa chakula.

Wavulana wadogo nao wameacha shule ili waweze kuzisaidia familia zao baada ya ng’ombe wao wote kufa kutokana na kiangazi.

Serikali ya Ethiopia inafanya kazi pamoja na mashirika ya misaada kugawa chakula hasa kwa watoto milioni 6 walio katika hatari ya njaa, magonjwa na ukosefu wa maji.

Kutokana na utapia mlo na ukosefu wa chakula, watoto wengi wanashukiwa kuwa na ukuaji mdogo wa ubongo na hali hiyo hatimaye itasababisha uwezo wao wa kufikiri na huenda ikawa mbaya zaidi.

Zaidi ya dola milioni 800 za dharura zimetolewa lakini serikali ya Ethiopia na Umoja wa Mataifa wanasema kuwa jumla ya dola bilioni 1.4 zinahitajika mwaka huu. Nyingi ya fedha hizo zitatumika kununua chakula.

Msaada wa chakula utahitajika Ethiopia hadi mwaka 2017 na sehemu nyingine za mashariki na kusini mwa Afrika nako hali ya kiangazi inashuhudiwa ikiaminika kusababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa maarufu El Nino.

XS
SM
MD
LG