Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 03, 2023 Local time: 08:00

Hali ya Madagascar ni ya kutatanisha


Wananchi wa Madagascar wakipanga foleni kupiga kura ya maoni.

Kundi la maafisa wa kijeshi huko Madagascar linasema limechukua udhibiti wa kisiwa hicho kilichopo kusini mashariki mwa Afrika.

Kundi la maafisa wa kijeshi huko Madagascar linasema limechukua udhibiti wa kisiwa hicho kilichopo kusini mashariki mwa afrika.

Kanali Charles Andrianasoavina alitoa taarifa kwenye kambi ya jeshi nje kidogo ya mji mkuu hii leo, wakati wapiga kura wakipiga kura juu ya rasimu ya katiba mpya. Alisema taasisi za serikali zimevunjwa na jeshi litaweka kamati ya kuongoza nchi.

Kanali huyo alikuwa ni mmoja wanajeshi waliokuwa wakimuunga mkono rais Andry Rajoelina, wakati Bw. Rajoelina alipochukua madaraka katika mapinduzi yaliyoungwa mkono na jeshi mwaka jana. Hakukuwa na majibu ya mara moja kwa tangazo hilo la jumatano kutoka kwa serikali ya Rajoelina.

Mashahidi wanasema hakuna ishara za moja kwa moja za jeshi kuipindua serikali kwenye mitaa ya mji mkuu wa Antananarivo.

XS
SM
MD
LG