Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 12:36

Hali ya kibinadamu yazidi kuzorota Syria


Moshi ukifuka katika majengo ya Syria.
Moshi ukifuka katika majengo ya Syria.

Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu lasema watu kadhaa waokolewa kutoka Homs.

Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu linasema wafanyakazi wa misaada wa Syria wamewaokoa watu kadhaa kutoka eneo la mji wa Homs lililozingirwa na majeshi ya serikali lakini wameshindwa kuokoa kundi la waandishi habari wa Magharibi waliokwama kwenye eneo hilo. Msemaji wa ICRC mjini Geneva anasema magari ya kubebea wagonjwa ya shirika la hilali Nyekundu yaliingia katika eneo linaloshikiliwa na waasi la Baba Amr Jumatatu, na kuokoa raia watatu wa Syria waliojeruhiwa.

Amesema wafanyakazi wa misaada walishindwa kuwaokoa wanahabari wa Magharibi, wawili kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya au kuopoa miili ya watu wengine waliouwawa kwenye mashambulizi ya risasi wiki iliyopita.

XS
SM
MD
LG