Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 13:06

Hali nchini Syria yazidi kuzorota


Moja ya majengo yaliyolipuliwa Damascus Jumamosi Machi 17, 2012

Mlipuko wa bomu wakumba mji wa Aleppo.

Bomu limelipuka katika mji wa Aleppo Jumapili , mji wa pili kwa ukubwa nchini Syria siku moja baada ya milipuko miwili katika mji mkuu Damascus kuuwa watu 27 na kujeruhi zaidi ya mia moja.

Idara rasmi ya habari nchini humo imesema mlipuko wa Allepo ulitokea kati ya majengo mawili ya makazi. Idara hiyo imeripoti kuwa shambulizi hilo ni kazi ya magaidi ambao serikali ya Syria inalaumu kwa upinzani na maandamano ya mwaka mzima dhidi ya rais Bashar al-Assad.

Kundi la ufuatiliaji la haki za binadamu juu ya Syria lenye makao yake Uingereza limesema mlipuko wa leo Jumapili umeuwa watu watatu na kujeruhi zaidi ya 25 na kwamba bomu hilo lilitegwa ndani ya gari karibu na jengo la ulinzi.

Katika milipuko ya Jumamosi mjini Damascus mabomu mawili yaliyotegwa ndani ya magari yalilipuka moja baada ya nyingine kwenye makao makuu ya kijasusi na jengo la ulinzi la maafisa wa polisi.

Umati mkubwa ulikusanyika Jumapili kwenye eneo la mlipuko huo kwa maombi. Serikali ya Syria na upinzani zinalaumiana juu ya mashambulizi hayo ya mabomu.

XS
SM
MD
LG