Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 04:02

Hali bado ngumu kupatikana spika wa bunge la Marekani


Jitihada za kiongozi wa chama cha Republican Kevin McCarthy kuwa spika ajaye wa Baraza la Wawakilishi la Marekani zilionekana kutowezekana Jumatano.

Jitihada za kiongozi wa chama cha Republican Kevin McCarthy kuwa spika ajaye wa Baraza la Wawakilishi la Marekani zilionekana kutowezekana Jumatano.

Kundi la wabunge wakonsevativ walizuia uungwaji mkono muhimu katika duru kadhaa za upigaji kura.

McCarthy, mwakilishi kutoka California, amekuwa akisaka uspika, lakini alishindwa mara tatu katika upigaji kura wa Jumanne katika jitihada ya kusaka kura 218 katika baraza lenye wajumbe 435, na alishindwa katika duru tatu nyingine za upigaji kura siku ya Jumatano.

McCarthy alipungukiwa na kura 17 Jumatano, huku wakonsevativ wa chama chake wakiendelea kusema hana nguvu za kutosha za kiitikadi kuongoza. Imepita miaka 100 kukosekana mshindi wa uspika kwenye duru ya kwanza ya upigaji kura kuwa spika.

XS
SM
MD
LG