Hatua hiyo ilichukuliwa tarehe 16 mwezi huu baada ya waziri mkuu Hailemariam Desalegn kutangaza kujiuzulu na siku mbili baada ya serikali kuachilia huru wapinzani wake pamoja na wakosaoaji wa kisiasa ikiwa sehemu ya programu ya kupunguza taharuki za kisiasa.
Ethiopia imeshuhudia ghasia za mara kwa mara kutoka kwa waandamanaji dhidi ya serikali tangu 2014 yaliochochewa na ugawaji wa madaraka miongoni mwa vyama vya kisiasa na vikundi vya kikabila.