Mgomo huo wa kitaifa unaingia katika wiki yake ya pili Jumatatu baada ya majadiliano ya mwishoni mwa wiki kati ya vyama vikuu vya wafanyakazi na serikali kushindwa kukubaliana juu ya kurudishwa ruzuku zilizondolewa tarehe 1 Januari.
Taarifa iliyotolewa na vyama viwili vikuu, NLC na TUC ilitolewa Jumapili kueleza kwamba mgomo utaendelea na kwamba kitisho cha kusitisha uzalishaji mafuta nchini Nigeria kimeondolewa.
Wakati wa mazungumzo ya Jumamosi wakuu wa vyama vya wafanayakazi walimtaka rais Goodluck Jonathan kurudisha ruzuku ya mafuta inayokadiriwa kugharimu serikali karibu dola bilioni 8 kwa mwaka. lakini serikali kwa upande wake iliahidi kupunguza bei za mafuta.
Mazungumzo hayo yalimalizika usiku wa manane bila ya makubaliano kufiiwa na haikujulikana ikiwa viongozi hao watakutana tena Jumapili.
Kabla ya ruzuku ya mafuta kuondolewa Wanigeria walikua wanalipa karibu senti 60 kwa lita moja lakini bei zilipanda na kufikia hadi $1:50 kwa lita moja.Bei za chakula na usafiri zimepanda pia.