“Haiti inathamini kitendo hiki cha mshikamano wa Afrika,” taarifa ya waziri wa mambo ya nje Jean Victor Geneus ilisema Jumapili, “na iko tayari kukaribisha ujumbe wa Kenya wa kutathmini hali uwanjani.”
Jumamosi, Kenya ilitangaza kuwa imejiandaa kupeleka maafisa 1,000 wa polisi kusaidia kutoa mafunzo kwa wenzao wa Haiti katika kupambana na magenge ya wahalifu ambayo yamedhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu, Port-au-Prince.
“Kenya imekubali kwa nia njema kuongoza kikosi cha kimataifa nchini Haiti,” ilisema taarifa ya Kenya, iliyochapishwa na waziri wa mambo ya nje Alfred Mutua.
Kenya kupeleka kikosi chake cha polisi bado itahitaji idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, vile vile makubaliano rasmi na mamlaka za Haiti.
Baraza la usalama lilimuomba katibu mkuu Antonio Guterres kuwasilisha ifikapo katikati ya mwezi Agosti ripoti kuhusu njia zinazowezekana kwa Haiti, ikiwemo ujumbe unaoongozwa na Umoja wa Mataifa.
Mutua alisema Kenya itatuma ujumbe wa kutathmini hali ilivyo nchini Haiti wiki ijayo.
Forum