Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, siku ya Alhamisi lilimthibitisha rasmi aliyekuwa waziri mkuu wa Ureno, Antonio Guterres kama katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa.
Katika umoja ambao ni nadra kwenye vikao vya baraza hilo, wanachama kumi na tano wa baraza walimuunga mkono guterres, ambaye aliongoza shirika la Umoja huyo la kuhudumia wakimbizi, na kumuidhinisha kwa kauli moja kuchukua usukani wa umoja huo, pale katibu mkuu wa sasa, Ban Ki Moon, atakapoondoka mwishoni mwa mwaka huu.
Balozi wa Urusi, Viatly Churkin, ambaye ndiye kiongozi wa mwezi huu wa baraza hilo, alitangaza matokeo ya kura hiyo rasmi hivi leo katiika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
Churkin alimuelezea guterrez kama mwanasiasa aliyebobea, na ambaye huzungumza na kila mtu na kumskiliza kila mmoja na kuelezea hisia zake waziwazi, na akaongeza kuwa anadhani guterres anafaa kuchukua wadhifa huo.
Guterres, mwenye umri wa miaka 67, alikuwa waziri mkuu wa Ureno kwa miaka kumi, kutoka mwaka wa 1992 hadi mwaka wa 2002 na alikuwa mkuu wa shirika la UNHCR kutoka mwaka wa 2005 hadi 2015.
guterres aliiambia VOA kwamba alikuwa anawania kiti hicho kwa sababu angependa kupata suluhisho kwa changamoto zinazoukabili ulimwengu.