Aliwaeleza wanahabari kwamba njia ya kwenda mbele iko wazi, ni kusimamisha mapigano mara moja kwa ajili ya juhudi za kininadamu.
Amesema pande zote mbili lazima ziheshimu wajibu wao chini sheria za kimataifa zinazosimamia juhudi za kibinadamu, na kwamba hakuna upande wa mgogoro ambao uko juu ya sheria hizo.
Hii anasema ni pamoja na kuachiliwa huru bila ya masharti mateka wote 240.
Guterres amesema kuheshimu sheria za kimataifa za juhudi za kibinadamu kuna maana ya kuwalinda raia, ikijumuisha kutokumia raia kama kizuizi cha vita, hospitali, maeneo ya Umoja wa Mataifa, na kujihifadhi, ikiwa pamoja na shule za Gaza, na kutaka kuongezwa kwa misaada na mafuta kwa eneo hilo linaloshambuliwa.
Forum