Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 03:40

Guterres apigwa na butwa kutokana na uharibifu unaotokana na mafuriko Pakistan


Katibu Mkuu Antonio Guterres akifuatana na waziri mkuu wa Pakistan Shahbaz Sharif akizungumza na watoto katika shule inayowapatia hifadhi.
Katibu Mkuu Antonio Guterres akifuatana na waziri mkuu wa Pakistan Shahbaz Sharif akizungumza na watoto katika shule inayowapatia hifadhi.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema Jumamosi, kwamba hajapata kushuhudia maishani mwake uharibifu mkubwa kutokana na hali ya hewa kama alivyoshuhudia janga lililosababishwa na mafuriko makubwa nchini Pakistan.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi habari mjini Karachi, Guterres amesema, “ nimeona maafa ya kibinadamu sehemu mbali mbali za dunia, lakini sijawahi kushuhudia uharibifu wa kiwango hiki kutokana na hali mbaya ya hewa. Kwa hakika sina la kusema kuelezea kile nilichokiona hii leo.”


Karibu watu 1 400 wamefariki kutokana na mafuriko yaliyofunika karibu theluthi moja ya ardhi ya Pakistan kutokana na mvua nyingi na kuharibu mimea, nyumba, majengo ya biashara, barabara na madaraja pamoja na kuwasababisha mamilioni ya watu kupoteza makazi yao.


Guterres amesema kwamba mataifa yanayoendelea yanapata hasara kubwa zaidi kutokana na dunia nzima kutegemea na kutumia mafuta ghafi.


Katibu mkuu ana matumiani kwamba ziara hiyo yake itaweza kuwahamisisha wafadhili kuchanga fedha kuisaidia Pakistan, ambayo inakadiria kwamba itahitaji zaidi ya dola bilioni 30 kwa kazi za kukarabati na kuwapatia wananchi makazi mapya.


Karibu watu milioni 33 wameathirika kutokana na mafuriko yaliyoharibu karibu nyumba milioni 2 na majengo ya biashara, na kubomoa kilomita elfu 7 za barabara na kuporomoka kwa madaraja 500.


Ofisi ya utabiri wa hali ya hewa inasema kwamba Pakistan imepata mara tano zaidi ya mvua mwaka huu wa 2022 kuliko ilivyokuwa kawaida.

XS
SM
MD
LG