Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 03, 2023 Local time: 04:29

Guterres aomba uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine usitishwe ili kudhibiti bei za juu za chakula


Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, April 5, 2022. Picha ya AP
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, April 5, 2022. Picha ya AP

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Antonio Guterres, Jumatano amesema uvamizi wa Russia dhidi ya Ukraine lazima usitishwe ili kukomesha kuongezeka kwa mizozo ya chakula, mafuta na fedha duniani, ambayo “inaweza kuwatumbukiza mamilioni ya watu zaidi kote ulimwenguni kwenye njaa na umaskini mwaka huu.”

“Vifo na uharibifu lazima visitiswe,” Guterres amewambia waandishi wa habari.

“Suluhisho la kisiasa lazima litafutwe kulingana na sheria za kimataifa na hati ya Umoja wa mataifa,” ameongeza.

Lakini hadi hilo litakapofanyika, amesema hatua ya haraka inahitajika ili kurejesha uthabiti wa chakula na masoko ya nishati duniani ili kupunguza kupanda kwa bei, uwezo unaohitajika upatikane ili kusaidia nchi maskini na jamii kukabiliana na athari za vita hivyo.

Guterres amekuwa akihusika katika juhudi za siri kujaribu kupata makubaliano ambayo yataruhusu usafirishaji wa chakula kinachozalishwa na Ukraine kupitia bahari nyeusi, na masoko ya kimataifa yaweze kupata chakula na mbolea kutoka Russia.

“Makubaliano hayo ni muhimu kwa mamilioni ya watu kutoka nchi maskini ikiwemo kusini mwa jangwa la Sahara,” Guterres amesema.

Lakini hakufafanua ikiwa timu yake inakaribia kufikia makubaliano hayo, kwa sababu amesema hataki kukwamisha fursa za mafanikio wakati ustawi wa mamilioni ya watu unategemea makubaliano hayo.

XS
SM
MD
LG