Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:54

Guterres: Nina wasiwasi mkubwa kuhusu Corona barani Afrika


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema Ijumaa kwamba ana wasiwasi kwamba iwapo virusi vya Korona vitasambaa kwa wingi barani Afrika, mamilioni ya watu huenda wakapoteza Maisha yao.

Alisema bara hilo halina mifumo na miundombinu ambayo inaweza kustahimili athari za virusi hivyo.

Katika mahojiano na shirika la habari la Marekani la PBS, Guterres alisema ni lazima mataifa ya dunia yashirikiane kwa karibu, katika vita dhidi ya Ugonjwa wa Covid-19, la sivyo, virusi hivyo vitakuwa na athari kubwa kwa binadamu.

"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu Afrika," alisema.

Umoja wa mataifa ulitangaza Ijumaa kwamba wafanyakazi wake wapatao 86 wameambukizwa virusi hivyo.

Marekani sasa imeipiku China katika idadi ya watu walioambukizwa, na kufikia Jumamosi asubuhi, ilikuwa imerekodi visa 104, 837, na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kadri Wamarekani wengi wanavyoendelea kufanyiwa vipimo.

Kwa mujibu wa kituo cha Johns Hopkins, China imerekodi takriban visa 82,000, huku Italia ikiwa na watu 86,000 walioambukizwa.

Kwa jumla, zaidi ya watu laki 6 duniani, wameambukizwa virusi hivyo.

-Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington DC

XS
SM
MD
LG