Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 03:14

Guinea yaripoti kifo cha kwanza kutokana na virusi vya Marburg

This negative stained transmission electron micrograph (TEM) depicts a number of filamentous Marburg virions. Authorities in West Africa have confirmed the region's first known case of Marburg virus after at least one person in Guinea died of the disease.

Maafisa huko Afrika Magharibi wamethibitisha kesi ya kwanza inayojulikana ya eneo hilo ya virusi vya Marburg baada ya  mtu mmoja nchini Guinea kufariki dunia

Maafisa huko Afrika Magharibi wamethibitisha kesi ya kwanza inayojulikana ya eneo hilo ya virusi vya Marburg baada ya mtu mmoja nchini Guinea kufa kwa ugonjwa wa homa ya kutokwa na damu Shirika la Afya Ulimwenguni limesema Jumatatu.

Maafisa wa afya walisema walikuwa wakijaribu kutafuta kila mtu ambaye alikuwa na mawasiliano na mgonjwa huyo ambaye alikwenda kutibiwa huko Gueckedou.

Kesi hiyo iliripotiwa katika sehemu ile ile ya Guinea ambapo ugonjwa wa Ebola wa mwaka 2014-2016 ulianzia ambao uliua watu wasiopungua 11,325. Mlipuko mwingine mdogo wa Ebola mapema mwaka huu pia ulipiga eneo hilo hilo karibu na mipaka ya Guinea na Sierra Leone na Liberia, na kusababisha watu 12 kufariki dunia.

XS
SM
MD
LG