Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 03, 2024 Local time: 22:32

Vyama vya wafanyakazi Guinea watowa wito wa mgomo kuendelea


Maduka ya mjini Conakry yamefungwa kutokana na mgomo wa kitaifa February 2024
Maduka ya mjini Conakry yamefungwa kutokana na mgomo wa kitaifa February 2024

Shughuli zote katika mji mkuu wa Guinea, Conakry zilisita kwa siku ya pili mfululizo Jumanne kutokana na mgomo uloitishwa na vyama vya wafanyakazi, siku moja kabla ya kiongozi wa Shirikisho la Wafanyakazi aliyekizuizini kukata rufaa.

Shule, maduka, na masoko yalifungwa huku barabara za Conakry zilikuwa tupu na hospitali zikitoa huduma za dharura.

Shirikisho la vyama vikuu vya wafanyakazi liliitisha mgomo tangu Jumatatu, likidai kupunguzwa kwa bei ya vyakula, kusitishwa kwa udhibiti wa vyombo vya habari, hali bora ya maisha kwa watumishi wa umma na kuweka shinikizo la kuachiwa kwa wanaharakati wa shirikisho.

Msemaji wa shirikisho Amadou Diallo ameiambia AFP kwamba, wamekuwa wakisubiri “hadi kuona matakwa yao yanatekelezwa kikamilifu" kabla ya kusitisha mgomo.

Aliongeza kusema kwamba hakuna mkutano ulopangwa na maafisa wa serikali siku ya Jumanne.

Vyama vya wafanyakazi vimefanya kuachiliwa huru kwa Sekou Jamal Pendessa, katibu mkuu wa Chama cha Waandishi Habari wa Guinea SPPG, kuwa sharti kuu kabla ya majadiliano yeyote na wakuu wa baraza tawala la kijeshi.

Waendesha bodaboda wakisubiri wateja mjini Conakry wakati wa mgomo wa kitaifa.
Waendesha bodaboda wakisubiri wateja mjini Conakry wakati wa mgomo wa kitaifa.

Pendessa alikamatwa mwisho wa mwezi wa Januari kwa "kushiriki kwenye maandamano ambayo hayakuruhusiwa" na siku ya Ijuma alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela ambapo miezi mitatu ni kifungo cha nje.

Kundi la mawakili wanaomtetea wanasema, wamepokea taarifa Jumatatu kwamba kesi yake ya rufaa itasikilizwa Jumatano.

Maandamano yamepangwa kutokana na kuongezeka kwa mivutano ya kijamii na ukosefu wa serikali ya mpito, baada ya Baraza la Kijeshi kutangaza kuvunja serikali hiyo wiki iliyopita bila ya kutoa sababu yeyote.

Katika maandamano ya Jumatatu watu wawili waliuliwa katika kitongoji cha Conakry.

Maandamano yamekua jambo nadra chinu ya utawala wa kiongozi wa kijeshi Jenerali Mamady Doumbouya, aliyechukua madaraka kufuatia mapinduzi ya Septemba 2021, na hatimae yalipigwa marufuku mwaka 2022.

Forum

XS
SM
MD
LG