Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 00:51

Guinea na Ivory Coast yawarudisha nyumbani raia wake  kutoka Tunisia


Raia wa Ivory Coast wanaoishi Tunisia na wanaotaka kurejeshwa nyumbani, wakisubiri nje ya ubalozi wa Ivory Coast mjini Tunis, Tunisia Februari 27, 2023. REUTERS
Raia wa Ivory Coast wanaoishi Tunisia na wanaotaka kurejeshwa nyumbani, wakisubiri nje ya ubalozi wa Ivory Coast mjini Tunis, Tunisia Februari 27, 2023. REUTERS

Mataifa ya Afrika Magharibi ya Guinea na Ivory Coast yanawarudisha nyumbani raia wake  wanaotaka kuondoka nchini Tunisia baada ya kiongozi wa nchi hiyo anayezidi kuwa  na utawala wa kiimla kutaka wahamiaji kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wasakwe.

Morissanda Kouyate, Waziri wa Mambo ya Nje wa Guinea na Waguinea wanaoishi nje ya Nchi, alikuwa ndani ya ndege ya kukodi iliyowarudisha Waguinea 49 hadi mjini Conakry Jumatano usiku, serikali ilisema. Wengine 81 wanangojea safari za ndege zijazo, aliongeza.

"Wenzetu wa Tunisia, tuligundua kuwa baadhi yao walikuwa wamepoteza matumaini," Kouyate alisema. "Na ni kwa moyo mzito kwamba niliweza kukutana nao kwa sababu hali ilikuwa ngumu."

Mama-aissata Sacko, mama wa watoto watatu, alisema familia yake imeshambuliwa na kuishi kwa hofu katika taifa hilo la Afrika Kaskazini.

“Hatukutoka kutafuta chakula. Mara tu unapotoka, wanakupiga mawe. Wanasema: Ondoka. Nendeni nyumbani, Tunisia ni ya Watunisia.' Mimi na watoto wangu tulikaa siku mbili bila kula," alisema aliporejea Guinea Jumatano.

XS
SM
MD
LG