Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 20:45

Majeshi ya usalama Guinea yazuia waandamanaji


Polisi wa kutuliza ghasia wakipambana na walinzi wa kiongozi wa upinzani Cellou Diallo, mara walipomkamata baada ya kulizuia kundi la Diallo kufanya maandamano huko Conakry, Guinea Set. 27, 2011
Polisi wa kutuliza ghasia wakipambana na walinzi wa kiongozi wa upinzani Cellou Diallo, mara walipomkamata baada ya kulizuia kundi la Diallo kufanya maandamano huko Conakry, Guinea Set. 27, 2011

Majeshi ya usalama nchini Guinea yamewazuia wafuasi wa upinzani kuandamana kuipinga serikali inavyoshughulikia suala la uchaguzi

Majeshi ya usalama Guinea yamezuia maandamano ya upinzani yanayopinga namna serikali inavyoshughulikia suala la uchaguzi ujao wa wabunge.

Wafuasi wa upinzani walipanga kufanya maandamano katika mji mkuu, Conakry, Jumanne lakini majeshi ya polisi na yale yanayopambana na ghasia yaliwazuia kujumuika pamoja.

Ushirika wa makundi ya upinzani unamshutumu Rais Alpha Conde, katika jaribio la kuipa kura za uchaguzi kuhakikisha anashinda ushindi mkubwa katika bunge. Uchaguzi unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Bwana Conde aliingia madarakani mwezi Disemba baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini Guinea tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1958.

Kufuatia maandamano yaliyopangwa, jeshi la Guinea liliamuru wanajeshi wake kukaa kwenye vituo vyao.

Jeshi limekuwa likishutumiwa kwa kushiriki katika mauaji ya umma yaliyotokea kwa waandamanaji wa upinzani. Jumatano ni maadhimisho ya miaka miwili ya mauaji ya umma yaliyotokea kwenye uwanja mmoja wa mpira wa Conakry, ambapo zaidi ya watu 150 waliuwawa.

Kundi moja la maafisa wa jeshi liliongoza nchi kwa wakati huo, baada ya kuchukua madaraka kwa miezi tisa.

Serikali hiyo ya muda iliongozwa na Jenerali Sekouba Konate, iliongoza nchi hadi uchaguzi wa urais ulipofanyika mwaka jana.

XS
SM
MD
LG