Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:39

Rais wa Guinea anusurika kifo


Rais wa Guinea anusurika kifo
Rais wa Guinea anusurika kifo

Rais wa Guinea Alpha Conde aliepuka jaribio la mauaji mapema Jumanne wakati watu wasiofahamika wenye silaha waliposhambulia nyumba yake.

Bwana Conde ambaye hakujeruhiwa katika tukio hilo baadaye alionekana kwenye televisheni ya taifa na alionekana kuwa shwari.

Mashahidi waliripoti kusikia milio mikali ya risasi mapema alfajiri kwenye nyumba ya Rais huko Kipe katika kitongoji cha mji mkuu Conakry. Katika hotuba yake bwana Conde alisema mapigano yalidumu kwa kiasi cha saa mbili na alimshukuru mlinzi wa rais ambaye alisema alipambana kufa.

Waziri mmoja katika serikali ya Guinea, Francois Fall anasema mlinzi mmoja aliuwawa.

Mashahidi huko Conakry waliiambia Sauti ya Amerika kuwa jeshi limefunga eneo kuzunguka nyumba ya bwana Conde. Hakuna madai yeyote ya mtu kuwajibika kwa shambulizi hilo.

Rais Conde alichukua madaraka miezi saba iliyopita baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini Guinea tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1958.

Taifa hilo tajiri lenye utajiri wa madini lina historia ya kufanyika mapinduzi ambapo mapinduzi ya karibuni yalifanyika mwezi Disemba mwaka 2008 baada ya kifo cha mtawala wa muda mrefu Lansana Conte.

XS
SM
MD
LG