Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 16:03

Rais wa Guinea Bissau afariki


Rais wa Guinea Bissau, Malam Bacai Sanha
Rais wa Guinea Bissau, Malam Bacai Sanha

Rais Sanha wa Guinea Bissau amefariki katika hospitali moja nchini Ufaransa

Rais wa Guinea Bissau, Malam Bacai Sanha amefariki dunia. Vyombo vya habari nchini humo vilitangaza Jumatatu kwamba Bwana Sanha alifariki katika hospitali moja mjini Paris, ambapo alikuwa amelazwa tangu mwezi uliopita.

Hakuna sababu zozote zilizotolewa juu ya kifo chake , lakini kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 64 alikuwa akipatiwa matibabu mara kwa mara nchini Ufaransa au Senegal tangu alipochaguliwa kuingia madarakani mwaka 2009. Alijulikana kuwa na ugonjwa wa kisukari pamoja na tatizo la damu mwilini mwake.

Kifo chake kimeongeza khofu kuhusu hali ya uthabiti nchini Guinea-Bissau, ambapo nchi hiyo ina historia ya kuwepo ghasia.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, darzeni ya wafanyakazi wa jeshi walikamatwa kwa kuhusika katika jaribio moja la mapinduzi. Watu waliokamatwa ni pamoja na mkuu wa jeshi la majini nchini humo, Bubo Na Tchuto, ambaye anashutumiwa kwa kuongoza mpango huo.

Bwana Sanha alichaguliwa kuchukua nafasi ya Rais Joao Bernardo Vieira, ambaye aliuwawa na wanajeshi waasi mwezi Machi, mwaka 2009.

XS
SM
MD
LG