Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:19

Goude ataka hoteli ya Ouattara ishambuliwe


Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wakifanya doria katika mtaa mmojawapo huko Abidjan, Ivory Coast. Dec 22,2010
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wakifanya doria katika mtaa mmojawapo huko Abidjan, Ivory Coast. Dec 22,2010

Waziri wa vijana katika serikali ya Ivory Coast anahimiza wafuasi wa Rais asiyetambulika kimataifa Laurent Gbagbo kuchukua udhibiti wa hoteli moja huko Abidjan, ambapo mpinzani wake Alassane Ouattara ameweka makao makuu chini ya ulinzi wa Umoja wa Mataifa.

Waziri Charles Ble Goude aliliambia gazeti moja la Ivory Coast siku ya Alhamisi kwamba bwana Ouattara ana hadi Januari 9 kuondoka hotelini hapo, ambapo ameunda serikali iliyotambuliwa kimataifa.

Ble Goude, ambaye pia anaongoza kundi la wanamgambo “Young Patriots” anataka lifanyike shambulizi la wazi katika hoteli hiyo.
Hoteli ya Waterfront inalindwa na kundi moja dogo la wapiganaji wa uasi wanaomtii bwana Ouattara na kiasi cha walinda amani 800 wa Umoja wa Mataifa.

Wote bwana Ouattara na bwana Gbagbo wanasema walishinda duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanyika Novemba 28. Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa inamtambua bwana Ouattara kama rais wa nchi hiyo.

Jumatano balozi mpya wa Ivory Coast katika Umoja wa Mataifa alisema mgogoro unaoendelea nchini humo kuhusu nani alishinda uchaguzi wa rais wa mwezi uliopita unachochea nchi kuingia katika mauaji ya halaiki.

Youssofou Bamba alitoa matamshi hayo huko New York baada ya kujitambulisha rasmi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon. Aliteuliwa kushika nafasi hiyo na bwana Ouattara.

XS
SM
MD
LG