Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 21, 2024 Local time: 20:16

Vifo vinavyotokana na pombe za kienyeji (gongo) Afrika Mashariki


Ramani ya Afrika Mashariki
Ramani ya Afrika Mashariki

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam limethibitisha kwamba watu 10 wamepoteza maisha mpaka sasa baada ya kunywa pombe ya kienyeji aina ya Gongo eneo la kimara Stop Over jijini humo.

Mtengenezaji na muuzaji wa pombe hiyo haramu inaripotiwa kuwa ametoweka. Hii si mara ya kwanza kwa pombe hii haramu kuuwa watu nchini humo na Afrika Mashariki, ikikumbukwa kuwa kumekuwa na matukio mbali mbali.

Gongo au chang'aa

Gongo au chang’aa ni kinywaji cha kienyeji ambacho hutumiwa zaidi ya vinywaji vingine kwa sababu ni bei rahisi ilikinganishwa na vinywaji vya ulevi mwengine.

Wachambuzi wanaeleza kuwa mamlaka katika mji wa Dar es Salaam inaonekana imeshindwa kuzuia vinywaji haramu. Kwa mujibu wa vyombo vya habari inaaminika kuwa pombe hiyo ilikuwa na kemikali maarufu kama GV , yenye rangi inayotumika kutibu maambukizi ya ugonjwa wa ngozi ambayo inadaiwa kusababisha vifo hivyo.

Jinsi inavyotengenezwa

Pombe hiyo ya kienyeji hutengenezwa kutokana na mbegu ama hata mboga nyumbani, pombe nyengine zinadaiwa kutengezwa kwa kutumia kemikali hatari kwa lengo la kuvifanya vinywaji hivyo kulevya zaidi na hivyo basi kuvutia wateja zaidi.

Waliokufa Kenya

Vile vile katika nchi jirani ya Kenya May 2014 Watu zaidi ya hamsini na tano walifariki dunia katika maeneo mbali mbali nchini humo baada ya kunywa pombe 'haramu'. Maeneo hayo yako katika mkoa wa kati na katika eneo la Mashariki mwa Kenya.

Mwaka 2015 aliyekuwa Gavana wa Murang’a Mwangi wa Irian a mwakilishi wa wanawake – Murang’a wakati huo Sabina Chege walifanya kampeni maalum ya kuangamiza vinywaji haramu. Vitaa hii iliongozwa na rais Uhuru Kenyata wa Kenya

Vifo hivyo vilitokea baada ya watu zaidi ya miamoja walibugia pombe haramu inayosemekana ilikuwa imechanganywa na kemikali aina ya Methanol ambayo ni sumu kwa mwili.

Maeneo hayo ni pamoja na majimbo ya Kiambu ambako watu 15 wamefariki, Jimbo la Embu Mashariki mwa nchi ambako wengine zaidi ya 20 wamefariki. Katika majimbo ya Kitui na Makueni mashariki mwa Kenya watu 20 wameripotiwa kufariki.

Kamanda wa Polisi

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kutokana na tukio la Alhamisi tayari uchunguzi umeanza baada ya kuchukua chupa tatu zenye kinywaji hicho cha pombe haramu aina ya Gongo eneo la tukio. Pia sampuli zimechukuliwa kutoka katika miili ya marehemu ambayo ipo katika hospitali ya mwananyamala pamoja na tumbi-kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Kamanda Lazaro ametoa wito kwa wananchi kuacha kushiriki katika unywaji wa pombe haramu zinazohatarisha maisha yao. Baadhi ya watu mashuhuda wa vifo vya Tanzania licha ya kudai idadi ya vifo ni kubwa zaidi ya kumi wamedai pia pombe hiyo ilichanganywa na kemikali kadhaa ikiwamo jiki , spiriti na safaru za shilingi tano na shilingi mia nia ikiwa ni kuongezea ukali

Tuhuma dhidi mmiliki wa gongo

Vyanzo vya habari vimesema kuwa mmiliki wa biashara hiyo haramu ya gongo aliyetajwa kwa jina la Mama Anoza, alianza kuwapeleka hospitali waathirika wa tuko hilo kimya kimya kabla ya kubainika chanzo cha mkasa huo na kwasasa ametoweka kama anavyozungumza kaimu mwenyekiti serikali ya mtaa stopover

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo la Stop Over wamezilaumu mamlaka husika wakiwemo polisi wanaodaiwa mara kadhaa kufanya opresheni na kukamata wahalifu ikiwemo mitambo ya gongo, bangi na mengineyo, kwa kushindwa kubaini biashara hiyo haramu katika eneo hilo, ambalo miaka ya 90 pia inadaiwa watu takribani 15, walipoteza maisha kufuatia kunywa pombe ya kienyeji aina ya Komoni.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Sunday Shomari, Washington, DC

XS
SM
MD
LG