Maandamano kadhaa katika mipaka ya israel ya kuunga mkono Wapalestina yaligeuka ghasia mbaya na kupelekea watu 10 kufariki dunia na mamia wengine kujeruhiwa.
Mashahidi na maafisa wa Lebanon wanasema majeshi ya Israel yaliuwa watu wapatao watano na kujeruhi zaidi ya hamsini wakati walipowafyatulia risasi waandamanaji ili kuwazuia kuvuka na kuingia Israel kutoka Lebanon.
Waandamanaji huko Syria pia walijaribu kuvunja uzio wa mpaka katika eneo linalokaliwa na Israel la milima ya Golan. Afisa mmoja wa Syria na mashahidi wamesema majeshi ya Israel yalifyatua risasi, kuuwa wanne na kujeruhi watu wapatao 45.