Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 17:34

Ghasia zamalizika hotel ya Hayat baada ya saa 30


Mlipuko wa mabomu ndani ya gari , Somalia
Mlipuko wa mabomu ndani ya gari , Somalia

Maafisa wanasema takriban watu 20 wameuwawa na shambulizi la risasi na mabomu wanamgambo na wengine 40 wamejeruhiwa.

Taarifa zinasema kuwa hoteli hiyo ya Hayat imeharibiwa vibaya kufuatia mapigano makali baina ya maafisa wa usalama na washambuliaji wanamgambo kuanzia Ijumaa usiku hadi Jumamosi.

Maafisa wa usalama wa somalia wamekuwa wakipambana na wanamgambo wa al shabab tangu walipovamia hoteli ya Hayat Ijumaa usiku , kwa mashambulizi ya mabomu na risasi , maafisa wamesema.

Raia wakiwemo wanawake na watoto waliokolewa katika hoteli hiyo wakati shambulizi linaendelea.

Hotel ya Hayat mara nyingi inakuwa na maafisa wa serikali , viongozi na watu kutoka jumuiya za kigeni.

Wafanyabiasha na viongozi wa ndani ni miongoni mwa waliouwawa na kujeruhiwa katika shambulizi hilo.

Kwa mujibu wa ndugu, mmiliki mwenza Abdirahman Iman ni miongoni mwa waliouwawa.

Kitengo maalumu cha operesheni za usalama kinachojulikana kama Alpha Group kilichopatiwa mafunzo na Marekani kiliingia katika ghorofa ya chini wakati washambuliaji wa risasi kutoka mbali wakiwa wameshika nafasi katika ghorofa za juu, kwa mujibu wa mashahidi.

Shambulizi lilianza Ijumaa baada ya sala ya jioni wakati gari lililokuwa na mabomu kulipuka lakika lango la kuingilia kwenye hoteli.

Milipuko mingine miwili ilifuatia na baadae mashambulizi ya risasi yalitulia baada ya polisi kuvamia hoteli hiyo, mashahidi wameeleza. Kundi la Al Shabab lenye uhusiano na al qaida limedai kuhusika na shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG