Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 15:13

Ghasia zakumba kampeni za uchaguzi Nigeria


Ghasia nchini Nigeria

Wafuatiliaji wa uchaguzi waeleza hofu juu ya ghasia nchini Nigeria

Wafuatiliaji wa uchaguzi nchini Nigeria wanasema ongezeko la ghasia za kisiasa hasa mashambulizi ya mabomu katika mikutano ya kampeni, huenda ikahujumu uchaguzi wa urais na wabunge mwezi ujao.

Ghasia na wizi wa kura yamekuwa mambo ya kawaida nchini Nigeria tangu mwaka 1999, pale taifa hilo lilipoondoka kutoka utawala wa kijeshi na kuingia katika utawala wa kiraia.

Ghasia hizo zimesabaisha vifo vya takriban watu mia tatu wakati wa uchaguzi wa mwisho uliofanyika mwaka 2007, ambao pia wasemekana uligubikwa na vitisho kwa wapiga kura na masunduku ya kura kujazwa kura za wizi na hivyo kusababisha uchaguzi huo kukataliwa na wafuatiliaji wengi wa kitaifa na kimataifa.

Sasa yakiwa yamesalia majuma kadhaa tu uchaguzi ufanyike na ambao waripotiwa kuwa wenye ushindani mkali kuwahi kufanyika, kundi la kutetea haki za biandamu -Human Rights Watch linasema ghasia za uchaguzi zimewauwa zaidi ya watu 50 tangu mwezi Novemba, na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka.

Nigeria inaelekea kufanya uchaguzi mwezi ujao, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa kiti cha rais hapo Aprili 9.

XS
SM
MD
LG