Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:03

Ghasia zaendelea Ukraine


waandamanaji wanaopinga serikali ya rais wa Ukraine Viktor Yanukovich katika Independence Square, Februari 19, 2014
waandamanaji wanaopinga serikali ya rais wa Ukraine Viktor Yanukovich katika Independence Square, Februari 19, 2014

Pamoja na vifo, takriban watu 300 wamelazwa hospitali wakiwemo polisi 88, waandishi habari na mbunge.

Mashahidi katika mji mkuu wa Ukraine wanasema watu wapatao 22 wameuwawa katika mapigano mapya yaliotokea kati ya waandamanji wanaopinga serikali na Polisi saa kadhaa baada ya rais Viktor Yanukovych kutangaza suluhu na viongozi wa upinzani.

Baadhi ya waliouwawa waliripotiwa kupigwa risasi na walenga shabaha wa serikali. Wakati huo huo wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine iliripoti polisi watatu waliuwawa Alhamisi. Imesema zaidi ya polisi 50 walilazwa hospitali jana, 30 kati yao wakiwa na majeraha ya risasi.

Ghasia baina ya polisi na waandamanaji zimeongezeka wiki hii. Pamoja na vifo, takriban watu 300 wamelazwa hospitali, wakiwemo maafisa wa polisi 88, waandishi habari 6 na mbunge mmoja.
XS
SM
MD
LG