Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 02, 2024 Local time: 04:38

Ghasia za kupinga matokeo ya uchaguzi Comoro za zidi kuwa mbaya


Wafuasi wa upinzani wakiiharibu picha ya rais aliye madarakani Azali Assoumani huko Moroni Januari 17, 2024. Picha na Olympia de Maismont/ AFP.
Wafuasi wa upinzani wakiiharibu picha ya rais aliye madarakani Azali Assoumani huko Moroni Januari 17, 2024. Picha na Olympia de Maismont/ AFP.

Ghasia za baada ya uchaguzi nchini Comoro zimekuwa mbaya siku ya Alhamisi wakati mtu wa kwanza kufariki baada ya kupigwa risasi, huku wanajeshi wakipambana na waandamanaji katika mitaa ya mji mkuu wa Moroni.

Mkuu wa chumba za dharura katika hospitali ya El Maarouf iliyoko, Moroni, Dr Djabir Ibrahim aliwaambia waandishi wa habari kuwa watu sita wamejeruhiwa na wamelazwa hospitali na kijana mwenye umri wa miaka 21 amefariki, “uwezekano mkubwa kwa kupigwa risasi”

Dokta Ibrahim anasema mmoja miongoni mwa waliojeruhiwa yuko katika hali mahtuti.

Taarifa za mwanzo za watu waliojeruhiwa vibaya zilijitokeza siku ya pili baada ya mamlaka ya uchaguzi kutangaza kuchaguliwa tena kwa Rais Azali Assoumani, na kuchochea vurugu na mapambano mitaani kati ya wanajeshi na wafuasi wa upinzani wenye hasira.

Akikaidi mvua nyingi na mabomu ya kutoa machozi kijana, mwenye umri wa miaka 20 hivi, akiwa amefunika uso wake aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi ni kwa nini ghasia zimezuka tena katika visiwa hivyo kwenye Bahari ya Hindi.

“Tumekuwa tukipigana kwa zaidi ya saa 24 kwa sababu hatukubaliani na matokeo ya uchaguzi. Ndiyo maana tunachoma majengo ya serikali.”

Vijana wamekuwa wakijaribu kuweka vizuizi barabarani na mitaani katika mji kuu wa Moroni, wakiwatupia mawe maafisa wa usalama, ambao wamekuwa wakijaribu kuwatawanya lakini vijana wamekuwa wakikimbilia vichochoroni na kuwasubiri.

Amri ya kutotoka nje usiku ilitangazwa Jumatano, lakini kufika asubuhi siku ya Alhamisi maduka na masoko yalikuwa bado yamefungwa na mji huo wa watu 100,000 ulikua mtupu.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP

Forum

XS
SM
MD
LG