Kundi hilo lakutetea haki za binadamu limesema ghasia za baada ya uchaguzi wiki iliyopita zimesababisha vifo vya takriban watu 500 na vikosi vya usalama vinajiandaa kwa uwezekano wa ghasia zaidi katika uchaguzi wa Jumanne wa serikali za mitaa.
Civili Rights Congress lilitangaza Jumapili kuwa sehemu kubwa ya ghasia hizo ziligubika majimbo ya kaskazini yenye waislam wengi, na Kaduna ikiwa ndio imeathirika zaidi.
Maafisa wa Nigeria wanakataa kutoa taarifa zozote za ghasia hizo. Lakini mashahidi wanaripoti kuona miili iliyotetekezwa barabarani na makanisa yaliochomwa moto.
Ghasia hizo zililipuka baada ya rais Goodluck Jonathan mkristo aliposhinda tena uchaguzi wiki iliyopita na kumshinda mgombea Muislam Muhammadu Buhari. Waunga mkono wa kiislam walifanya ghasia za kuwapinga wakristo na wakristo wakalipa kisasi.
Bw Buhari anapinga matokeo hayo, lakini wafuatiliaji huru wanasema kwa sehemu kubwa uchaguzi ulifanyika kwa njia ya huru na haki.
Majimbo kadhaa ya Nigeria yameanda kufanyika kwa uchgauzi wa magavana siku ya Jumanne. Wakuju wa usalama wanajaribu kuwahakikishia raia kwamba watakuwa katika hali ya usalama na wajitokeze kupiga kura.