Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 04, 2022 Local time: 20:17

Ghasia za kidini zaongezeka Jamhuri ya Afrika ya Kati


Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu waondoa maiti kwenye kaburi la pamoja mjini Bangui, Feb. 17, 2014.

Kundi la wanamgambo wanaojiita anti- balaka linawalenga waislam katika mji mkuu Bangui.

Afisa wa juu wa Umoja wa Mataifa anasema ghasia za kidini zinazoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya kati zinaonekana kuwa mbaya zaidi.

Katika taarifa Jumatano kamishna anayehusika na maswala ya haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Navi Pillay alisema ukiukwaji mwingi wa haki unaendelezwa na kundi la wanamgambo wanaojiita anti-balaka ambao amesema kwamba wanalenga kwa maksudi waislam katika mji mkuu Bangui.

Pillay amesema wanamgambo hao wanauwa na kuwabaka waislam na kuharibu nyumba zao na wana nia ya wazi ya kuwazuia waislam kurudi kwenye makazi yao.
XS
SM
MD
LG