Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 20:15

Ghasia nchini Kenya zimesababisha mashaka kukidhi malengo ya IMF


Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF
Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF

Mswada huo ulijumuisha ushuru usiopendwa na umma kwenye mkate, mafuta ya kupikia na sukari

Maandamano ya ghasia ambayo yalimlazimisha Rais wa Kenya William Ruto auondoe mswada wa fedha, umesababisha mashaka kwa nchi katika juhudi za kukidhi malengo ya shirika la kimataifa la fedha-IMF na kufanya ukopaji kuwa wa gharama kubwa sana, wawekezaji na wachambuzi wamesema.

Mswada huo ulijumuisha ushuru usiopendwa na umma kwenye mkate, mafuta ya kupikia na sukari, gharama za uhamishaji wa pesa kwenye mitandao ya simu, na baadhi ya uagizaji bidhaa kutoka nje. Ulikusudiwa kukusanya shilingi bilioni 346 za Kenya sawa na dola 2.68 bilioni, au asilimia 3 ya Pato la jumla la Taifa, katika mapato ya ziada, Morgan Neville Z. Mandimika wa Stanley aliandika katika barua.

Kuondolewa kwa mswada huo huenda kutasababisha Kenya kukosa asilimia 4.7 ya lengo la nakisi mwaka huu na asilimia 3.5 mwaka ujao kulingana na kwa mpango wa IMF, alisema.

IMF haikutoa tamko lolote mara moja iwapo itawezekana kubadilisha malengo yanayohitajika kwa Kenya. Lengo letu kuu katika kuisaidia Kenya ni kuisaidia kushinda changamoto za kiuchumi zinazowakabili na kuboresha matarajio ya kiuchumi na ustawi wa watu wake, msemaji wa IMF Julie Kozack amesema katika taarifa.

Forum

XS
SM
MD
LG