Polisi wa kutuliza ghasia nchini Congo walifyatua mabomu ya machozi kwa wafuasi wa upinzani baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa jana Jumapili.
Dazeni ya polisi walifukuza watu nje ya vituo hivyo vya kupigia kura katika mji mkuu Brazaville wakati kazi ya kuhesabu kura ilipoanza katika uchaguzi ambao unatarajiwa kuwa kiongozi wa muda mrefu Denis Sassou Ngueso kuongeza utawala wake wa miongo mitatu.
Katika mkesha wa upigaji kura serikali iliamuru makampuni ya simu kusitisha huduma zote wakati wa upigaji kura.
Waziri wa mambo ya ndani wa Congo, Raymond Zefirin Mbulu, aliandika waraka kwa makampuni makuu mawili ya simu akisema kwa sababu za usalama wa taifa walisitisha ikiwa ni pamoja na ujumbe wa maandishi kwa Jumapili na Jumatatu.