Polisi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo wamefyatuliana risasi na watu wasiojulikana hivi leo katika tukio kubwa la kwanza la ghasia tangu kuchaguliwa tena kwa Rais Denis Sasou Nguesso mwezi uliopita.
Mapambano hayo yalitokea katika mitaa ya Brazaville kwenye maeneo ya Bacongo na Makeleke. Hakujapatikana ripoti za majeruhi.
Taarifa kutoka serikali zinasema wanamgambo wa zamani waliokuwa na silaha "Ninja", ambao waliwahi kumtii baba wa mgombea aliyeshindwa katika uchaguzi wa mwezi uliopita, walishambulia na kuchoma moto kituo cha jeshi cha Mayanga, vituo vinne vya polisi na ofisi ya meya kusini mwa Brazaville.
Nguesso alichaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo 1979 na 1992 na baada ya kushindwa uchaguzi alirudi tena madarakani 1997. Alishinda uchaguzi uliopingwa 2002 na 2009 kabla ya kupata ridhaa ya wapiga kura kuondoa vipengele kwenye katiba ambavyo vingemzuia kugombea katika uchaguzi wa Machi 20 kwasababu ya umri na ukomo wa kugombea.