Ghana imefikia makubaliano ya kimsingi na makundi mawili ya wadhamini ili kufanyia kazi tena dola bilioni 13 deni la kimataifa na kukata asilimia 37, alisema siku ya Jumatatu, ikikaribia lkukamilisha marekebisho ya deni ambayo kwa miaka mingi yamekuwa yakifanyiwa kazi. Chini ya makubaliano, wamiliki wa dhamana watasamehe karibu dola bilioni 4.7 ya madai yao na kutoa misaada ya mtiririko wa fedha
Dola Bilioni 4.4 katika kipindi cha hivi sasa cha mpango wa mkopo wa Ghana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ambao unatarajiwa kuhitimishwa 2026.
Mkataba huo utaipatia Ghana njia ya kufufua uchumi kupitia misaada muhimu ya madeni na utoaji wa mtiririko wa fedha, Kamati inayowakilisha wadhamini wa kimataifa ilisema katika Taarifa ya kukaribisha mkataba huo. Hii ni habari njema kwa nchi, alisema Theo Acheampong,
Mchambuzi wa mahesabu katika S&P Global Market Intelligence. Kwa kweli imekuwa haraka zaidi kuliko wenzao kama vile Zambia na inapaswa kusaidia kupunguza deni la umma na kufungua Zaidi rasilimali za kutumia katika maeneo ya ukuaji wa kipaumbele kama vile kilimo na miradi ya miundombinu iliyokwama, alisema.
Forum