Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:25

Ghana yakabiliwa na uhaba wa umeme


Rais wa Ghana John Dramani Mahama.
Rais wa Ghana John Dramani Mahama.

Ukosefu wa nguvu za umeme umetokea kwenye taifa la pili kwa ukubwa katika eneo la Afrika magharibi la Ghana.

Ukosefu wa nguvu za umeme umetokea kwenye taifa la pili kwa ukubwa katika eneo la Afrika magharibi la Ghana huku Rais John Dramani Mahama akilaumu wazalishaji wa mafuta katika Niger Delta nchini Nigeria.

Uchumi wa Ghana uliwahi kukua kwa haraka katika eneo hilo,lakini ukosefu wa umeme wa mara kwa mara, Serikali kutumia fedha zaidi pamoja na kuanguka kwa bei za bidhaa zinazotoka nchini humo zimepelekea Shirika la Fedha Duniani, IMF kutoa msaada wa dola bilioni moja kama njia ya kuokoa uchumi.

Rais Mahama amezungumzia tatizo lililoanza mapema mwaka huu baada ya kundi la wanamgambo kwa jina la Niger Delta Avengers, kuanza kuharibu mabomba yakusafirisha mafuta pamoja na vifaa muhimu katika eneo la Niger Delta ambapo Ghana inaagiza mafuta yake.

XS
SM
MD
LG