Mpinzani mkuu kwenye uchaguzi wa rais nchini Ghana amesema ana Imani kuwa atashinda huku akisihi wafuasi wake kuwa na subira wakati tume ya uchaguzi inapoendelea kukamilisha kazi yake.
Nana Akufo Addo alizungumza na wafuasi hao Alhamisi mjini Accra wakati tume ya uchaguzi ikianza kutoa matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa Rais na Bunge uliofanyika jumatano kupitia ujumbe wa Twitter.
Chama kikuu cha upinzani cha NPP kutokana na hesabu zake tayari kimetangaza Akufo Addo kuwa mshindi huku vyama vingine vitano vya upinzani vikifuata nyayo. Hata hivyo Rais alieko madarakani John Mahama pamoja na chama chake cha NDC hawajakubali kushindwa. Tume ya uchaguzi imesema kuwa inaamini upokeaji matokeo kwa njia ya elektroniki ulikuwa na matatizo na kwamba itatoa matokeao tu pale itakapo pokea nyaraka kwa njia ya mkono kutoka kwenye vituo.