Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 06:52

Gereza la wafungwa wa kisiasa limeshambuliwa huko Myanmar


Shambulizi la mabomu leo Jumatano huko Myanmmar karibu na lango kuu la kuingia kwenye gereza kuu ambalo wafungwa wa kisiasa wanazuiliwa limesababisha vifo vya watu wanane wakiwemo wageni na wafanyakazi wa gereza, vyombo vya habari vya ndani na serikali wamesema.

Watu watano ambao walikuwa wakipeleka vifurushi kwa wafungwa na wafanyakazi watatu wa gereza waliuawa wakati mabomu mawili yaliyolipuka kiasi cha tatu na dakika asubuhi kwa saa zahuko. News of Myanmmar mtandao wa habari ambao umeelemea kwenye sserikali ya kijeshi, uliripoti kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram.

Milipuko ilitokea ndani na nje ya ofisi ya kupokea wageni karibu na lango kuu la gereza la Insein mjini yangon, mji mkubwa nchini humo.

Ofisi ya habri ya kijeshi imethibitisha taarifa hiyo kwa kusema kwamba wageni watano, akiwemo msichana wa miaka 10 na wafanyakazi watatu wa gereza hilo waliuawa na bomu ambalo halikulipuka liligundulika kwenye moja ya vifurushi.

Taarifa ilisema wageni 13, pamoja na mvulana wa miaka 9, na wafanyakazi watano wa gereza walitibiwa kwa majeraha katika hospitali ya kitongozi cha Insein.

XS
SM
MD
LG