Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 22:06

Rais wa zamani George HW Bush alazwa hospitali


Rais George H. W. Bush.
Rais George H. W. Bush.

Msemaji wa Rais wa zamani wa Marekani, George H. W Bush amesema kuwa mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 92 alipelekwa hospitali mwishoni mwa wiki akisumbuliwa na tatizo la kushindwa kupumua.

Msemaji Jim Mc Grath amesema katika barua pepe aliyoituma kwa shirika la habari la Associated Press kuwa Bush amepata nafuu baada ya kupatiwa matibabu na madaktari wanaridhishwa na hali yake jinsi inavyoendelea hivi sasa.

McGrath amesema rais aliye na umri mkubwa kuliko marais wote wanaoishi hivi leo Marekani alipelekwa hospitali Jumamosi na anategemea kuruhusiwa kwenda nyumbani muda si mrefu.

Bush alikuwa rais wa Marekani kati ya mwaka 1989 na mwaka 1993. Ana maradhi ya “Parkinson” na amekuwa akitumia kiti chenye kuendeshwa na mota.

XS
SM
MD
LG