Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:54

Gavana wa jimbo Aghanistan auwawa na bomu la kujitoa muhanga


Serekali ya Taliban, nchini Afghanistan, Alhamisi imesema kuwa mlipuko wa bomu katika ofisi ya gavana wa jimbo, umemuua yeye na wengine wawili.

Shambulio la asubuhi huko Mazar-i-Sharif, mji mkuu wa jimbo la kaskazini la Balkh, lilijeruhi takriban watu saba, kwa mujibu wa maafisa wa hospitali ya eneo hilo.

Maafisa wa polisi wa jimbo wamesema kuwa mwanamume aliyekuwa amevaa mabomu alijilipua kwenye ghorofa ya pili ya jengo la ofisi ya gavana aliyeuawa, Mohammad Dawood Muzamil.

Hakuna aliyedai mara moja kuhusika na shambulio hilo baya.

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid kwenye Twitter alithibitisha kifo cha Muzamil, akisema aliuawa akiwa shahidi katika mlipuko wa maadui wa Uislamu, na kwamba uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG