Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 23:11

Gavana wa Florida atangazwa Seneta mteule


 Gov. Rick Scott wa jimbo la Florida ndiye seneta mteule baada ya kumshinda Mdemokrat Bill Nelson.
Gov. Rick Scott wa jimbo la Florida ndiye seneta mteule baada ya kumshinda Mdemokrat Bill Nelson.

Gavana wa jimbo la Florida wa chama cha Republican, Rick Scott, Jumapili alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa seneti dhidi ya mpinzani wake mdemocrat, Bill Nelson, kufuatia kuhesabiwa tena kwa kura  kwa kutumia mkono baada ya zaidi ya wiki moja tangu ufanyike uchaguzi wa katikati ya muhula.

Matokeo hayo yanaonyesha Scott aliongoza kwa tofauti ya kura elfu 10. Baada ya uchaguzi wa Novemba 6, Scott alikuwa anaongoza kwa kura elfu 15, ikiwa ni chini ya asili miya 0.5.

Sheria ya uchaguzi ya Florida inalazimisha kura zihesabiwe tena kwa mashine iwapo mgombea atamshinda mpinzani wake kwa tofauti ya chini ya asili miya 0.5.

Sheria hiyo inazitaka kura kuhesabiwa kwa mkono iwapo mshindi alipata chini ya asili miya 0.25. Scott aliyeungwa mkono na Rais Trump wakati wa kampeni, yeye binafsi na Trump waliwashtumu wasimamizi wa operesheni ya kuhesabu kura kutaka kufanya njama za wizi ili mpinzani wake kutoka chama cha democrat aweze kushinda.

Tuhuma hizo zilitupiliwa mbali baada ya kuonekana kwamba hazina msingi.

Bill Nelson, aliyekua anashikilia kiti cha seneta wa Florida kwa tikiti ya chama cha democratic tangu mwaka wa 2000 amekiri kushindwa.

Scott ambaye amekuwa gavana wa Florida tangu 2011 amempongeza Nelson kwa kukubali matokeo ya uchaguzi.

Baada ya ushindi huo wa Scott, chama cha Republican sasa kinaongoza kwa viti 52 kwenye baraza la seneti dhidi ya viti 47 vya Wademocrat. Kiti cha seneti katika jimbo la Mississipi bado kina utata na duru ya pili ya uchaguzi itafanyika Novemba 27, ya kumtafuta mshindi.

-Imeandikwa na mwandishi wa VOA, Patrick Nduwimana

XS
SM
MD
LG