Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 11:02

Gambia: Mkuu wa zamani wa ujasusi apatikana na hatia ya mauaji ya mpinzani mashuhuri


Rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh, akiondoka kwenye kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa rais, mjini Banjul, Disemba 1, 2016, picha ya Reuters
Rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh, akiondoka kwenye kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa rais, mjini Banjul, Disemba 1, 2016, picha ya Reuters

Jaji mmoja nchini Gambia Jumatano alimuweka hatiani mkuu wa zamani wa ujasusi na maafisa wengine wa ujasusi kwa mauaji ya mwaka 2016 ya mwanaharakati wa kisiasa muda mfupi kabla ya uchaguzi ambao ulisaidia kumaliza utawala wa dikteta Yahya Jammeh.

Jaji wa mahakama kuu Kumba Sillah Camara alimkuta na hatia mkuu wa zamani wa idara ya kitaifa ya ujasusi (NIA), Yankuba Badjie, ya kumua Ebrima Solo Sandeng, mwanachama mashuhuri katika chama cha upinzani cha United Democratic Party (UDP).

Badjia alipatikana pia na hatia ya kudhuru mwili.

Mkuu wa operesheni katika idara hiyo ya ujasusi, Sheikh Omar Jeng, pamoja na maafisa wa idara hiyo Babucarr Sallah, Lamin Darboe na Tamba Mansary walikutwa na hatia kwa mashtaka hayo hayo.

Sandeng alikamatwa wakati wa maandamano ya Aprili 2016 dhidi ya Jammeh. Alifariki mbaroni siku mbili baada ya kupigwa na kuteswa.

Kifo chake kilichochea vuguvugu la kisiasa ambalo hatimaye lilimuondoa madarakani Jammeh, ambaye alikuwa ametawala taifa hilo dogo la Afrika magharibi kwa miaka 22.

XS
SM
MD
LG