Mwanasheria mkuu Dawda Jallow, amesema kwamba mwendesha mashtaka maalum atasimamia kesi za matumizi mabaya ya madaraka wakati wa utawala wa Jammeh, kati yam waka 1994 na 2017.
Kesi hiyo zimeorodheshwa katika ripoti ya tume ya ukweli na maridhiano iliyozinduliwa mwaka uliopita.
Tume hiyo huru ilisema kwamba Jammeh na watu aliokuwa nao serikalini, walihusika na makosa ya uhalifu 44, yakiwemo mauaji na unajisi, dhidi ya waandishi wa habari, wanajeshi, na wanasiasa wa upinzani.