Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:26

Gambia yatoa adhabu kali kwa wasafirishaji madawa


Mitungi iliyosadikiwa kujazwa madawa
Mitungi iliyosadikiwa kujazwa madawa

Mahakama moja nchini Gambia imewahukumu raia wanane wa kigeni kifungo cha miaka 50 kila mmoja kwa kusafirisha madawa

Mahakama moja nchini Gambia imewahukumu raia wanane wa kigeni kifungo cha miaka 50 jela kila mmoja, kwa kujaribu kusafirisha zaidi ya tani mbili za madawa ya kulevya aina ya cocaine kupitia nchi hiyo ya Afrika magharibi.

Jaji alisema Jumatano anataka kutuma ujumbe kwa wasafirishaji madawa wengine kwamba Gambia ni eneo lisiloingilika.

Washukiwa hao wanne ni raia wa Venezuela, wawili wa Uholanzi, mmoja wa Nigeria na mmoja wa Mexico. Muda mfupi kabla ya hukumu kutolewa, afisa mmoja katika jela aliiambia mahakama kwamba raia mmoja wa Venezuela alikufa gerezani Jumapili kwa sababu za kawaida.

Polisi nchini Gambia waliwakamata washukiwa hao mwaka jana katika kijiji kidogo cha uvuvi karibu na mji mkuu, Banjul. Maafisa wa usalama wanasema walificha Cocaine chini ya ukuta wa uongo ndani ya ghala. Polisi wanasema madawa hayo yalikuwa yakisafirishwa kwenda ulaya.


XS
SM
MD
LG