Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 20:40

Gadhafi bado hajulikani alipo


Wapiganaji wa kundi la waasi wa ki-Taureg wa Niger MNJ wakiendesha magari yenye silaha kaskazini mwa Niger.
Wapiganaji wa kundi la waasi wa ki-Taureg wa Niger MNJ wakiendesha magari yenye silaha kaskazini mwa Niger.

Maafisa wa Niger wamekanusha ripoti za vyombo vya habari kwamba magari 200 ya kijeshi kutoka Libya yameingia nchini humo, wanasema ni magari matatu tu yaliyovuka mpaka.

Habari za kutatanisha zilianza kutokea Jumanne jioni kuhusiana na ikiwa wafuasi wa Gadhafi wamevuka mpaka na kuingia katika nchi jirani ya Niger au la.

Gazeti la Marekani, "The New York Times" limemnukuu waziri wa sheria wa Niger, Marou Amadou akisema, msafara huo ulikuwa ni wa magari matatu tu na kwamba hayakupakiza silaha.

Mkuu wa kikosi cha usalama wa bwana Gadhafi, Mansour Dhao na washauri wake kadhaa ndio watu pekee waliovuka mpaka na kuingia.

Shirika la habari la Associated Press-AP limemnukuu mkuu wa utawala wa Rais wa Niger, Massoudou Hassoumi akisema kwamba, wakati bwana Dhao alipovuka mpaka alisindikizwa hadi mji mkuu wa Niamey na hivi sasa anashikiliwa katika nyumba moja katika mji huo.

Bwana Hassoumi anasema mashahidi walioripoti kuona msafara mrefu wa magari hawakufahamu kulikuwepo na magari yaliyopelekwa na serikali ya Niger kuwapokea na kuwasindikiza wa-Libya hao.

Awali iliripotiwa kwamba msafara huo wa magari ulikuwa unalindwa na wapiganaji wa kundi la waasi wa kabila la Taureg kutoka Niger.

Wakati huo huo serikali ya nchi jirani ya Niger upande wa kusini magharibi, Burkina Faso imekanusha ripoti kwamba imekubali kumpatia Gadhafi hifadhi ya ukimbizi.

Kwa upande wake waziri wa ulinzi wa Marekani Leon Panetta aliwaambia waandishi wa habari kwamba Washington haijui mahala kiongozi huyo wa zamani wa Libya alipo. Anasema wanachofahamu ni kwamba Gadhafi yupo katika harakati za kuondoka nchini humo.

XS
SM
MD
LG