Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 04:58

Dereva wa lori auwa zaidi ya watu 70 Ufaransa


Lori lililouwa watu mjini Nice Ufaransa

Dereva wa lori mjini Nice Ufaransa Alhamisi jioni aliendesha gari hilo kwenye umati wa watu mjini Nice Ufaransa.

Dereva wa lori mjini Nice Ufaransa Alhamisi jioni aliendesha gari hilo kwenye umati wa watu waliokuwa wakisherehekea siku kuu ya Uhuru wa Ufaransa na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 70 huku wengine zaidi ya mia wakijeruhiwa.

Wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa iliothibitisha vifo hivyo ilisema kuwa dereva huyo alipigwa risasi na kuuwawa na polisi.

Msimamizi wa vipindi wa VOA Linda Ringe aliekuwa kwenye eneo la tukio alisema aliona miili mingi ikiwa imetanda barabarani.

Haijadhibitishwa kama tukio hilo ni la kigaidi lakini mamlaka zinasema kuwa dereva huyo aliendesha gari hilo kwa maksudi.

Rais wa Ufaransa aliitisha mkutano wa dharura kwenye ofisi za wizara ya mambo ya ndani .

XS
SM
MD
LG