Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 06:01

Vyama vya wafanyakazi Ufaransa vyatishia kuendelea kufanya migomo zaidi


Wafanyakazi wanaogoma wakiifunga njia ya kuingilia ghala ya mafuta ya shirika la Total mjini Donges, magharibi mwa Ufaransa.
Wafanyakazi wanaogoma wakiifunga njia ya kuingilia ghala ya mafuta ya shirika la Total mjini Donges, magharibi mwa Ufaransa.

Mgomo wa usafiri umekuja siku kadhaa tu kabla ya kufunguliwa kwa michuano ya kandanda ya Europa hapo Juni 10.

Ufaransa inatarajia migomo mipya wiki hii, wakati rais Francois Hollande anakataa pendekezo la serikali la mageuzi ya ajira ambalo limechochea miezi ya migomo na maandamano kote nchini.

Baadhi ya vyama vya wafanyakazi nchini Ufaransa ikiwa ni pamoja na shirikisho kuu la wafanyakazi CGT vimeitisha migomo mipya ambayo italenga usafiri wa treni, mfumo wa usafiri mjini Paris, bandari na hata viwanja vya ndege.

Jana jumanne , mamia ya waandamanji waliziba njia ya kuingia eneo linalotumiwa na magari makubwa karibu na Marseille.

Kiongozi wa CGT, Olivier Mateu aliwaambia waandishi wa habari kuwa pengine serikali ilipuuza upinzani kwa mswaada wa mageuzi ya ajira.

Olivier Mateu mwenye umri wa miaka 42 ni kiongozi wa CGT mjini Marseille. Anasema serikali ilitegemea kuwa kuingia kwa msimu wa machipuko na hali ya hewa ya joto, taifa lote litakuwa limelala. Kwa hakika hili halitatokea. Sasa lazima alichukulie kwa dhati, na sisi tunasema hili mara kwa mara. Hakuna aibu kwa kiongozi wa siasa pale unapofanya kosa, kurudi nyuma na kubadili uwamuzi wako, na kubuni hali ili tuweze kuzungumzia maendeleo ya kijamii katika taifa hili.

Waandamanaji walizuia usafiri wa magari makubwa ya biashara katika eneo la mpito karibu na Marseille kwa saa chache jana.

Mgomo wa usafiri umekuja siku kadhaa tu kabla ya kufunguliwa kwa michuano ya kandanda ya Europa hapo Juni 10, ambayo inatarajiwa kuvutia mamillioni ya wageni nchini ufaransa, hiyo itaongeza matatizo yalosababishwa na vizuizi kwenye vya wiki iliyopita kwenye ghala za mafuta.

Takriban vinu 11 kati ya vinu 58 vya nishati ya nuklia vya Ufaransa vilikumbwa na matatizo bila kupangwa pale wafanyakazi wake walipojiunga katika migomo.

Wiki ilopita waziri mkuu Manuel Valls alipendekeza mabaliko au kuuboresha mswaada ambao ungefanya iwe rahisi kwa waajiri, kuajiri na kuwafuta kazi wafanyakazi wake na kudhoofisha nguvu za vyama vya wafanyakazi, lakini badala yake serikali haitouacha mswaada huo.

Wakati huohuo katika nchi jirani ya Ubelgiji, wafanyakazi wa sekta ya umma wamesitisha huduma za usafiri wa umma kwa kugoma dhidi ya makato ya bajeti hio jana, na hivyo kuzidisha shinikizo kwa serikali ambayo tayari inakumbana na migomo ya wafanyakazi wa magereza na wa usafiri wa reli.

XS
SM
MD
LG