Chama cha mrengo wa kulia nchini Ufaransa kimeshindwa kupata ushindi katika uchaguzi, licha ya kupata nafasi ya juu katika duru ya kwanza ya upigaji kura.Ubunifu wa upigaji kura wa wapinzani wa National Front umesaidia kuwanyima uongozi.
Wafuasi wa chama cha National Front walionyesha bayana hisia zao pale matokeo yalipokuwa yakitiririka kutoka kote nchini Ufaransa. Licha ya kushinda katika maeneo 6 kati ya 13, katika duru ya kwanza, chama hicho kilishindwa kupata udhibiti wa eneo lolote kati ya maeneo 13 katika upigaji kura wa wa jumapili.
Lakini mchambuzi Marta Lorimer wa shule ya uchumi mjini London anasema matokeo yana umuhimu.
Anasema wakati huohuo wamepata idadi kubwa ya kura katika historia yao. Ni chama ambacho kina historia ya miaka 40 na wamefikisha takriban kura millioni 7.
Kiongozi wa National Front Marine Le Pen akizungumza kwa sauti ya kikaidi
Le Pen anasema, ulimwengu wanashughulikia kuvunjika kwa Ufaransa na watu wake na kuwa taifa kubwa lenye mkusanyiko wa watu. Anasema Sisi wazalendo tunatumai kuwa taifa hili linalinda nafasi ya wafaransa.
Ufaransa bado ingali katika hali ya dharura takriban mwezi baada ya kundi la Islamic State kufanya mashambulizi ya kigaidi kote mjini Paris, ambayo yalipelekea watu 130 kuuwawa. Lakini hofu ya ugaidi wa waislamu wenye msimamo mkali hauelezi kuongezeka kwa umaarufu wa National Front.
Bi Lorimer anasema, wanashinda katika maeneo mengi ambayo kihistoria hupigia kura chama cha kikomunisti na cha mrengo wa kushhoto. Watu wengi ambao hawashindi kutokana na utandawazi, ambao si wazalendo, lakini bado wanahisi mambo yalikuwa bora pale Ufaransa ilikuwa ikijishughulikia yenyewe na haikuwa kuhusu Ulaya au ulimwengu.
Marine Le Pen aliaahidi wafuasi wake kuwa chama chake kitarejea na nguvu Zaidi mwaka 2017 ambapo anataraji kuwania nafasi ya rais nchini Ufaransa